Afrika iwe makini inaposhirikiana au kusaidiwa na nchi zilizoendelea
Manage episode 422164684 series 1226838
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, mataifa ya Ulaya, Amerika, Asia na sasa Uarabuni, yameongeza kasi ya uwekezaji, utoaji wa mikopo na misaada kwa nchi za Afrika, mataifa haya yamewekeza mabilioni ya dola za marekani kwa bara hilo kwa kubadilishana na rasilimali zake, hatua ambayo mbali na kuonekana kama ni urafiki lakini inaibua maswali kuhusu nia hasa ya nchi hizo kwa bara la Afrika.
Ni juma hili tu, Korea Kusini kwa mara ya kwanza imefanya kongamano na viongozi wa Afrika, ambapo imetangaza msaada wad ola za marekani bilioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na biashara kati yake na nchi hizo.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia kasi hii mpya ya nchi za magharibi kwa bara la Afrika, tukijiuliza maswali kadhaa, je nia yao ni safi? Na vipi Afrika inaweza kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi?
24 حلقات