Kenya: Namna mabaki ya ngozi ya samaki yanavyotumiwa kuhifadhi mazingira
Manage episode 432603373 series 1146275
Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Hata hivyo wenyeji sasa wengi wao vijana wameanza kutumia taka hizo kutengeza bayogesi na bidhaa zingine kama vile viatu,nguo,begi mifuko na kadhalika hivyo kubuni ajira na kuinua uchumi.
Katika fuo za Dunga kando na ziwa Victoria kaunti ya kisumu nchini Kenya,wafanyabiashara hapa wanatumia bayogesi kukaanga samaki na kuwauzia wateja wanaotalii êneo hili.Bayogesi hii inayotengenezwa kutokana na mabaki ya samaki ,imewafaidi wenyeji wa hapa kupunguza gharama ya matumizi vile vile kutunza mazingira. Caroline Achieng ni mfanyabiashara wa samaki.
“Tunadumisha usafi kwa sababu wageni wanakuja hapa lazima tudumishe usafi ndio mazingira yetu yasiharibike,mradi huo umesaidia sana kwa sababu wametusaidia kuchukuwa hizi takataka za samaki kama matumbo,wanatengeneza nayo bayogasi hivyo kupunguza uchafu”alisema Caroline Achieng mfanyabiashara wa samaki.
Kwa mujibu wa Achieng, uwepo wa mradi huu umeimarisha biashara yake ukilinganisha wakati alipokuwa akitumia kuni kukaanga samaki.
“Changamoto tuko nayo ni kama samaki haiko kwa sababu mazingira yameharibika,tudumishe usafi tutengeneze mazingira ili samaki ipate kuzalishana baharini.”AlisisitizaAchieng.
Mita chache kutoka kwenye wafanyabiashara hawa wanaokaanga samaki,Mary Dede ni mwenye furaha,Kwa sasa anatumia kawi inayotokana na bayogesi vile vile kawi mbadala,kukausha samaki aina ya dagaa kwa minajili ya kuwahifadhi kwa mauzo ya baadaye.
“Hapo tunaweka Omena kama tunataka kuikausha na inaweza chukuwa hata masaa tatu kukauka.”Alisema Mary Dede.
Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.
Mradi huu wa kutengeneza gesi kutokana na taka hizi umeimarisha mazingira na biashara ya hapa. Charles Ochieng ni mtaalam wa kutengeneza bayogesi kwenye shirika flexy biogás, shirika ambalo linaendesha mradi huu wa gesi êneo hili.
“Huwa tunachukuwa mabaki ya samaki ikifika jioni tunachukuwa tunaichunga maji yake tunamwaga kwa mtungi huu wa bayogesi, hiyo ndio inatengeneza bayogesi,uchafu mwingine tunatengeneza chakula ya kuku na nguruwe.” AlielezaCharles Ochieng ni mtaalam wa kutengeneza bayogesi.
Kwa siku kilo 300 za mabaki ya samaki hukusanywa hapa na kisha kuchakatwa kwa kimombo recycle kisha kuzalisha gesi ambayo kwa mujibu wa Ochieng huuzwa kwenye soko hili na mikahawa karibu.
“Bayogasi hii ,akina mama wanakuja hapa hapa wanapika githeri,omena na samaki na vyakula vingine ,wanalipa na inalingana na kiwacho cha chakula wanapika,ada ya juu zaidi ni shilingi 100 ,ada ya chini ni shilingi 50,tumsaidia eneo hili kutunza mazingira kwa vile uchafu huu sasa haurudishwi baharini.” AlisemaCharles Ochieng.
Takwimu kutoka taasisi ya Utafiti wa Baharini na Uvuvi nchini Kenya zinaonyesha kuwa tani 150,000 za taka za samaki huzalishwa kila mwaka, ambapo asilimia 80 ya taka hizo hutupwa na kuharibu mazingira .Samuel Okoth ni mtaalam wa mazingira jimbo hili la Kisumu.
“Ngozi hii na taka zingine zamani zilikuwa zinatupwa baharini na kuchafua mazingira,ndio tukagundua inaweza tengeneza bayogasi na bidhaa zingine kama viatu ,begi na vile vile kuunda uzi za kushona watu wakati wa upasuaji.”Alisimulia Samuel Okoth ni mtaalam wa mazingira jimbo hili la Kisumu.
Okoth anasema kuwa Ufumbuzi wa teknojia umesaidia sana kutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na taka hizi, hivyo kuajiri vijana wengi eneo hili.
“Bidhaa hizi kama begi hatuuzi hivi hivi tu tunauza katika masoko ya kimataifa kwa sababu dhamani yake ni ya juu mno,kwa sababu huo mchakato wa kuziunda ni ghali mno kama vile kulainisha hiyo ngozi ya samaki na kuifanya kuwa kubwa.”
Kilomita 6 kutoka ufuo huu wa dunga ni ,kijiji cha kajulu kaskazini mwa mji wa Kisumu,,namkuta Sarah Adero akitumia ngozi na magamba ya samaki kutengeza bidhaa kama vile nguo,viatu.magamba haya na ngozi ya samaki hukusanywa kutoka vituo mbalimbali jijini Kisumu .
“Ngozi hizi tunazitoa maeneo kama vile ubunga,tunazileta hapa na kuzilainisha na kuzitumia kutengeneza bidhaa tofautitofauti,ngozi hii ikiachwa tu hivyo itachafua mazingira hata kule baharini kisha samaki wengine wataweza kufariki.”
Mipango kama hii hata hivyo imeonekana kuchangia uchumi endelevu yaani circular economy hasa katika miji mbalimbali nchini Kenya, huku mashirika ya kaboni yakisema kuwa, fumbuzi hizi zitachangia Zaidi ya ajira millioni nane barani Afrika.
“Inaleta mapato sana na nawaambia wenzangu,kila kitu ina kazi,kama hii ngozi ya samaki mtu hawezi jua eti inaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali,ingetupwa ingechafua mazingira na pia hatungepata mapato.”
Uwepo wa hatua kama hizi za kutumia taka kutengeneza bidhaa mbalimbali ni moja wapo ya mataifa kama vile Kenya ,kuafikia malengo ya ruwaza ya maendeleo endelevu ya mwaka wa 2030 ,ambapo mataifa yanafaa kutumia uvumbuzi na teknolojia ili kutatua changamoto za mazingira,hivyo kubuni nafasi za kazi na kuimarisha mazingira.
Victor Moturi,Kisumu RFI Kiswahili.
24 حلقات